news, breaking news, news blog, business, sports,story, politics, technology, entertainment, living
Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Wednesday, June 13, 2012
Friday, March 23, 2012
ASPIRINI INAWEZA KUZUIA SARATANI
![]() |
| Vidonge vya Asprin |
Kumeza kidonge cha aspirini kila siku inaweza kuzuia na hata kutibu saratani. Taraifa hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya.
Matokeo
ya utafiti huo yalichapishwa na jarida la matibabu la The Lancet, na
hivyo kuzidisha kuonyesha manufaa ya aspirini katika matibabu ya
saratani.
Watu wengi tayari wanatumia Aspirini kama dawa ya maradhi ya moyo.
Lakini
wataalamu wanaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuelezea watu
kutumia aspirin ili kuzuia saratani na hata vifo vinavyotokana na
saratani.
Wataalamu hao wanaonya kuwa dawa hiyo inaweza kusababisha athari kubwa kama kuvuja damu tumboni.
Prof
Peter Rothwell,wa chuo kikuu cha Oxford akiwa na wakufunzi wengine
ambao wamefanya utafiti wa hivi karibuni, tayari walikuwa wamehusisha
aspirin na kuzuia aina ya saratani hasa saratani ya matumbo.
Lakini
utafiti wao wa awali, ulipendekeza kuwa watu wanahitaji kutumia dawa
hiyo kwa takriban miaka 10 ili iweze kufanya kazi hiyo.
Sasa
wataalamu wanaamini kuwa uwezo wa dawa hiyo kuzuia saratani, hutokea
mapema mno kati ya miaka mitatu na mitano. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
mpya kutoka kwa majaribio 51 yaliyohusisha wagonjwa 77,000.
Na
asprini haionekani tu kuzuia tisho la kuugua aina nyingi ya saratani
bali pia lakini pia inazuia saratani kusambaa kwa sehemu zingine
mwilini.
Hata hivyo majaribio hayo hayakufananisha dawa ya aspirini na dawa zengine zinazoweza kuzuia maradhi ya moyo.
Lakini
wakati kikundi cha wataalamu, kilichoongozwa na Profesa Rothwel
kilidurusu wangapi kati ya watu waliohusika katika utafiti huo walipata
kuugua saratani na hata kufariki kutokana na ugonjwa huo, waligundua
kuwa vifo vilitokana pia na matumizi ya aspirin.
Kuzuia kusambaa kwa Saratani
Kwa
mtu anayetumia kiwango kidogo cha dawa hiyo kila siku, ilionekana
kupunguza idadi ya visa vya saratani kwa robo baada ya miaka mitatu
pekee.
Ni
watu tisa waliogungulika kuwa na saratani katika watu elfu moja kila
mwaka ikilinganishwa na watu kumi na mbili kwa watu elfu moja kwa wale
waliomeza tembe hizo.
Pia ilipunguza idadi ya vifo vilivyookana na saratani kwa asilimia kumi na tano.
source:BBC
Saturday, March 3, 2012
REMEMBER MICHAEL
JE, ulikuwa na umri wa miaka mingapi wakati mfalme wa muziki wa Pop wa Marekani, hayati Michael Jackson alipoitembelea Tanzania mwaka 1992 na kufika shule maalum ya watoto yatima na wenye mtindio wa ubongo iliyopo Sinza?
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu zaidi duniani hadi anakufa 2009, alifika nchini akiwa balozi wa ziara ya Umoja wa Mataifa na akapokelewa kiserikali na Waziri wa Mambo ya Nje wakati huo, hayati Hassan Diria.
Michael Jackson alitua jioni moja uwanja wa ndege wa Dar akiwa amevalia shati la kijani lenye mikono mirefu, suruali nyeusi na kofia nyeusi, akapandishwa kwenye Mercedes iliyompeleka hadi Kilimanjaro Hotel (wakati huo) ambayo baadaye ikawa Kilimanjaro Hotel Kempinsk, sasa ikiitwa Hyatt Regency Dar es Salaam.
Pia, mashabiki waliokuwa na habari za ujio na ratiba yake, walijitokeza kwa wingi na kumshangaa vilivyo, The Wacko Jacko alipotembelea shule hiyo ya Sinza, kesho yake.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, alikutana na mkuu wa nchi ambaye wakati huo alikuwa Rais Ali Hassan Mwinyi.
Ndivyo Michael Joseph Jackson alivyofika Tanzania na kushikana mikono na watoto wa Sinza miaka karibu 20 iliyopita!
Wednesday, February 29, 2012
CHADEMA NA CCM KAMA REPUBLICAN NA DEMOCRATC

Inavyoanza
kuonekana kwa sasa vyama hivi pekee ndivyo vitakuwa vikimenyana kwenye
chaguzi kubwa.ni kama marekani.Naambiwa kule japo kuna vyama vingi sana
vidogo hata vya kikomunisti,lakini nyote mnajua kuwa kwa karne sasa ni
Republicans na Democrats pekee wanaotawala hasa siasa za nchi
hiyo.Mwenendo ulivyo kwa sasa hapa nchini Ni CHADEMA na CCM. Tangu
uchaguzi wa 2005 dalili hizi zilianza kuonekana hasa bungeni ambapo
ungedhani kulikuwa na wabunge wa vyama hivyo pekee.japo CUF kiliongoza
upinzani bungeni lakini kwa maoni yangu ni wabunge wa CHADEMA wale 11
waliojenga taswira ya upinzani.uchaguzi wa 2010 umeiweka CHADEMA kuwa
Kambi rasmi ya upinzani pamoja na sarakasi za Hamad Rashid na Kafulila
ambazo zilishindwa.
Mnaokumbuka
tena katika chaguzi zote ndogo tangia 2005, ni CHADEMA na CCM ndo
vimekuwa na ushindani wa kweli.Mnakumbuka
kiteto,Tarime,Biharamulo,Busanda,Mbeya Vijijini,Igunga,Uzini,na sasa
Arumeru? baadhi ya vyama vimekosa hata pumzi ya kuingia kwenye uchaguzi.
Kwa
hiyo hakuna haja ya kuunganisha vyama vya upinzani kama ilivyokuwa
inasemwa na baadhi ya watu hata wasomi.vyama vinaweza kuungana mkono tu
na siyo kuungana.vilevile hakuna haja ya kuogopa kusajili vyama vipya
kwani hata vikiwa 1000 itabaki kuwa CHADEMA Vs CCM.Kweli tunakoelekea ni
kuzuri
Mdau
KWA NINI WASICHANA HUBABAIKIA WENYE MAGARI NA FEDHA?
Ndio maana madereva wengi hasa wale wa teksi wanajisifu kwamba wanawake wanawapapatikia sana.
Je hili lina ukweli kiasi gani?
Lakini je ni wasichana wote ambao wanawapapatikia madereve au watu wenye magari?
Nadhani hili ndilo swali gumu sana kwenye suala hili
Kila kitu kinachohusu uhusianao wa kimapenzi, tunajifunza kutoka kwa wazazi au walezi wetu, labda asilimia 10 tu ndio tunayojifunza nje ya nyumbani.
Siyo suala la gari peke yake, bali ni suala la karibu kila kitu. Je watoto wetu tunawajengea dhana gani kuhusu kila kitu kwenye maisha?
Halafu tunawaambia kitu gani kuhusu kupenda?
Siku zote na tulio wengi tunawaambia watoto wetu uongo mwingi sana, na uongo huo unatokana na sababu nyingi.
Kwanza nasi tulidanganywa na wazazi wetu. Pili hatujiamini. Tatu hatuna uhakika sisi ni akina nani, na nne tunadhani uongo huo utawasaidia watoto wetu.
Hebu chunguza kwa makini utagundua kwamba, wasichana wanaobabaikia magari ni wale ambao wamelelewa kwenye malezi ya uongo mtupu.
Unaweza kudhani wale waliotoka kwenye familia masikini ndiyo ambao wanababaikia magari, hapana.
Msichana anaweza kutoka kwenye familia masikini na asibabaikie utajiri wala magari, wako wengi wa aina hiyo.
Kama nyumbani wazazi wanawasifu wenye magari, wanaonesha kwamba ukiwa na gari ndio unakuwa na maana, kwamba ndio kiwango cha juu cha mafanikio, unatarajia kitu gani kutoka kwa watoto?
Kuna wakati wazazi wanasema , “ameshafika mbali sio mwenzio, yule ana akili sana. Ana magari mawili na nyumba tatu.
Wakati mwingine inatosha mara moja tu, jambo kusemwa na mzazi, na mtoto kuamini kwamba mwenye gari au magari na nyumba ndiye aliyekamilika, ndiye mwenye akili..
Kumbuka mtoto anaingiza maarifa akilini mwake kutoka kwa watu anaowaamini anaokutana nao maishani. Kwenye suala la uhusianao wazazi ndio wanaoaminika zaidi.
Kwa sababu ya umasikini wetu, tulio wengi na uhaba wa malengo makubwa kuliko sisi wenyewe, gari na nyumba ndio malengo ya juu kabisa ya binadamu kuyapata.
Mtoto anakuwa na akili ya aina hiyo, kigezo chake kuhusiana na mtu kitakuwa ni gari, nyumba au mali kwa ujumla.
Kwake binadamu mwenye maana na anayefaa ni yule anayemudu kumiliki vitu hivyo.
Hii sio kwa wasichana peke yake bali hata wanaume. Kama mtoto wa kiume alioneshwa kuwa thamani ya mtu inatoka kwenye gari, nyumba na mali, basi naye atakuwa anababaikia vitu hivyo.
Linapokuja swala la uhusianao, atajitahidi kumuonesha msichana kwamba anavyo vitu hivyo au anao uwezo wa kuvimiliki. Anafanya hivyo kwa sababu aliambiwa thamani yake inakuwepo pale anapokuwa na vitu hivyo.
Wazazi wengi wameegemeza thamani zao kwenye vitu badala ya wao wenyewe. Bila ya hiyari yao wanawafundisha watoto wao kujali na kuthamini vitu badala ya utu wao.
Kwa kadiri mfumo wa maisha wa mitaji ulivyokuwa ukiendelea, binadamu alijitoa thamani na kuiweka kwenye vitu, hasa mali.
Kwa bahati mbaya wale watoto wa wazazi ambao wana maisha ya kati ndio ambao wanasumbuliwa na mali.
Kwa nini?
Kwa sababu wazazi wao hawajui kama wako juu au chini kimapato.
Katika kujitafuta hutoa kauli zenye kuonesha kwamba maisha ni mali, basi.
Wazazi walio na kipato cha chini nao wanaweza kuwaathiri vibaya watoto wao, kwa kuzungumza na kutenda katika njia ambayo watoto wataamini kwamba umasikini huondoa kabisa thamani ya mtu.Wale walio juu kabisa wanaweza wasifikirie kwamba gari au nyumba ni mambo ya maana sana, hata kama wamefundishwa kuhusu mali. Wao watafikiria mali kwa mkabala mkubwa zaidi.
Labda watafikiria kuhusu ndege au kutembelea boti ya kifahari na mengine, lakini wote watakuwa na udhaifu ule ule wa kuamini kwamba mali ni kubwa kuliko thamani ya binadamu.
Mali ambayo unaitengeneza na kuitafuta mwenyewe halafu iwe kubwa kuliko wewe! Hii ni ajabu kabisa.
Wazazi ambao wanachukulia mali kama kitu cha kawaida sana, ambacho uwe nacho au usiwe nacho, maana ya maisha haibadiliki, na thamani yako haiondoki kamwe, hawa ndio watoto wao watakuwa na maisha bora.
Monday, February 20, 2012
Wednesday, February 15, 2012
MIUNDO MBINU INAVYOLETA TABU DAR.
Tatizo la miundo mbinu limeendelea kuwa sehemu ya maisha katika jiji la Dar.
Monday, February 13, 2012
VALENTINE DAY.
![]() | |
| mtakatifu valentine |
Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo mtakatifu valentine au Valentinus. Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari. Mtakatifu Valentinus alipinga jambo hili hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru kukamatwa kwa Valentinus na kuuwawa.
Kuna hadithi ya kuwa akiwa gerezani mtakatifu Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani, mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya (From your Valentine). Toka hapa valentine anakumbukwa kama mtetezi wawapendanao na siku hii kuadhimishwa kote duniani
![]() | |
| ishala ya upendo baina ya mke na mme |
![]() | |
| wapendanao |
Thursday, February 9, 2012
MATOKEO KIDATO CHA NNE: JINSI MWANAFUNZI ALIVYOANDIKA BONGO FLEVA KWENYE MTIHANI
.
Katibu mtendaji mkuu wa baraza hilo Dr Joyce Ndalichako amesema mmoja kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo alifikia hatua ya kuandika mashairi ya bongo fleva baada ya kukosa cha kujibu ambapo aliandika “nashukuru sana wote wanaosahihisha huu mtihani wangu, nitakapofeli nitaendelea na fani yangu ya bongo fleva, majita yangu yako levo za juu na sio East zuu, ukiona vyaelea ujue vimeundwa”
Joyce amesema mtahiniwa aliandika mistari katika kila sehemu alipotakiwa kujibu swali, swali la sita na la saba aliandika hiyo mistari hapo juu, swali la kumi na moja ameandika “acha utani my girl, unauja nyumbani umezizi, mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”
kwenye sentensi nyingine Katibu huyo mkuu amesema “katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana watahiniwa laki mbili na elfu 25 sawa na asilimia 53.37 wamefaulu huku kati yao wasichana ni elfu 90 na 885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni laki moja na elfu 34 sawa na asilimia 57.51.
Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Francis Mbeya imeongoza kwa shule kumi zilizofanya vizuri, ambapo katika wanafunzi waliofaulu vizuri sana wameongozwa na Moses Andrew Swai kutoka shule ya sekondari ya Feza iliyopo jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)





