![]() |
| Joshua Nassari |
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemchagua Joshua Nassari
kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki,
utakaofanyika Aprili Mosi, mwaka huu.
Akitangaza
matokeo ya uteuzi huo, Mkurugenzi wa Bunge na Oganaizesheni wa Chadema,
John Mrema alisema Nassari ameteuliwa baada ya kupata kura 805 sawa na
asilimia 90.6 ya kura zote 888 zilizopigwa.
Alisema
Nassari aliwaangusha Anna Mghiwa aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata
kura 23, akifuatiwa na Godluv Simba (18), Rebecca Magwisha (12), Samweli
Shami (10), Anthony Mussari (8) na Yohanne Kimuto (6).
“Kura
zilizopigwa zilikuwa 888 zilizoharibika ni sita na wagombea wote
wametangaza kukubali matokeo,” alisema Mrema. Msimamizi wa uchaguzi huo
alikuwa ni mwasisi wa chama hicho, Edwin Mtei.
Ukumbini
Mgombea
Musari aliyehamia Chadema baada ya kuangushwa kwenye mchakato wa
kutafuta mgombea kupitia CCM aliwaambia wajumbe kwamba, tayari
alikwishafukuzwa kazi ya ukuu wa shule hivyo aliomba wajumbe wampigie
kura kupeperusha bendera ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini katika
uchaguzi huo.
Kauli
ya mgombea huyo ilimfanya mmoja wa wajumbe kutoka kata ya Maji ya Chai
kumhoji iwapo hatahama tena Chadema akikosa kura katika uchaguzi huo wa
jana, naye akaahidi kushirikiana na wana Chadema wenzake kutafuta
ushindi wa chama chake hicho.
Awali, mzee Mtei alisema chama hicho kinahitaji wabunge wenye kuendesha na kutekeleza sera zinazojibu mahitaji ya
wananchi
na jamii wanayoongoza kwa kuhakikisha rasilimali za taifa
zinawanufaisha wananchi wote bila kujali tofauti miongoni mwao.
“Hivi
sasa wananchi wengi wanakula mlo mmoja kwa siku sababu hawawezi kumudu
gharama ya milo miwili na hili linasababishwa na usimamizi na uongozi
mbovu wa Serikali ya CCM,” alisema Mtei.
Aliwaasa
wana Arumeru kupuuza rushwa inayodaiwa kuwa imeanza kusambazwa sehemu
mbalimbali za jimbo hilo na wanaodaiwa kuwa viongozi au wanachama wa CCM
na kuchagua kiongozi wanayeamini kuwa atawakilisha hoja na fikra zao
bungeni bila kushaiwishiwa kwa rushwa.
CCM wakamatwa kwa rushwa
Katika
hatua nyingine, viongozi watatu wa CCM, wanashikiliwa na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma za kujihusisha na
vitendo vya rushwa kuhusiana na kura za maoni za marudio ndani ya chama
hicho.
Kura za maoni zinatarajiwa kupigwa leo na wagombea wawili
walioongoza
katika awamu ya kwanza ya kura za maoni zilizofanyika wiki iliyopita,
Siyoi Sumari na Wililiam Sarakikya watapigiwa kura.
Kamanda
wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Mbengwa Kasomambuto alithibitisha jana kwa
simu kushikiliwa kwa viongozi hao ambao hata hivyo, alikataa kuwataja
majina kwa sababu ya kiuchunguzi.
“Kweli
tunawashikilia wana CCM watatu kwa mahojiano baada ya vijana wangu
waliotapakaa kila sehemu ya Jimbo la Arumeru Mashariki kuwakuta katika
mazingira yanayoashiria uwepo wa rushwa,” alisema...Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

No comments:
Post a Comment