Baadhi
ya wagonjwa waliopo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili wakisubiri
huduma katika Kitengo cha Mifupa (MOI), huku wakiwa hawajui hatma yao
baada ya madaktari kuanza mgomo wao kwa mara nyingine tena leo.
ULE
mgomo wa madaktari uliotangazwa kufanyika leo umeanza katika mazingira
ya kimyakimya. Hii imebainika pale mpekuzi wetu alipotembelea hospitali
hiyo ili kujionea kile kichokuwa kimekusudiwa.
Hali
ilivyokuwa katika hospitali hiyo kuu ya taifa kwa siku ya leo ni
kwamba hakuna daktari hata mmoja aliyekuwa anashughulika na mgonjwa bali
manesi tu ndiyo waliokuwa wanashughulika na wagonjwa wa zamani na si
wapya ambapo.
Uchunguzi
uliofanywa hospitalini hapo ni kuwa kila idara ilikuwa na mikutano
katika kujadili hotuba ya waziri mkuu aliyoitoa jana ikiwa inalenga
kuwasihi madaktari waache mgomo bali waendelee kufanya kazi huku suala
lao likiwa linashughulikiwa.
Kwa
upande wa madakari hao wameazimia kwa pamoja kuwa mgomo huo unaanza
rasmi leo baada ya kikao hicho na kuwataka wananchi wawaelewe kuwa
lengo lao ni kuboresha maslahi yao.
Kwa
mara nyingine Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema kama wanakusudia
kufanya mgomo huo basi serikali imejiandaa kwa kila hali ili
kukabiliana na mgomo huo.
Katika
mazingira ambayo yanaweza kuitwa tata siku ya kesho haileweki hali
itakuwaje kitu ambacho wagonjwa wengi wamepewa tarehe za mbele hali
ambayo wengi wao imesononeshwa na ahadi hizo.
Mpekuzi
wetu alipojaribu kumtafuta msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Ameniel Aligalesha, aliambiwa kuwa yupo katika kikao ndani ya hospitali
hiyo na lengo lilikuwa ni kujadili na kufikia maamuzi ya hotuba ya
waziri mkuu.
Hadi
leo Pinda ameishakaa mikutano mbalimbali kujadili swala hilo la
madaktari. Kwa mara ya kwanza ilikuwa Januari 29 mwaka huu katika
ukumbi wa Karemjee aliposema kuwa daktari ambaye angegome
angejifukuzisha kazi na akapiga marufuku mikutano yao kufanyika kokote.
Februari 9 alikutana na madakari bingwa na watumishi wa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Muhimbili.
Na
jana alikutana na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo aliyakataa
masharti ya madaktari ambayo waliyatoa ili waweze kuendelea na
mazungumzo na serikali.
Baada ya madaktari kukaa leo, Pinda amesema kama wametangaza mgomo serikali iko tayari kukabiliana na mgomo huo.
No comments:
Post a Comment