ANIKA
ALIVYOSHIRIKI KATIKA MCHAKATO KIPINDI AKIWA WAZIRI MAMBO YA NJE, ASEMA
ALIKUTANA NA MAMA MWENYE NYUMBA NA KUAGIZA ALIPWE DOLA MILIONI MOJA
HARAKA, AKAMPA OFA KUJA MBUGA YA NGORONGORO
Tausi Ally
ALIYEKUWA
Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu ameiambia
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Rais Jakaya Kikwete wakati akiwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alifahamu kuwepo kwa
rasimu mbili za mikataba ya ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania,
Italia.
Profesa
Mahalu alisema hayo jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta wakati
akitoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi na
kuisababishia Serikali hasara ya Euro 2,065,827.60 pamoja na aliyekuwa
Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.
Akiongozwa
na wakili wake, Mabere Marando, Profesa Mahalu aliitambua barua ya
Februari 20, 2002 ambayo ilikuwa ikieleza kuwa matayarisho yote ya
ununuzi wa jengo la ubalozi huko Italia yamekamilika ikiwa ni pamoja na
rasimu mbili za mikataba.
Mahalu
alidai kuwa katika mchakato wa ununuzi wa jengo hilo wakati yeye akiwa
Balozi chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
kulikuwa na rasimu mbili za mikataba na kwamba aliwahi kuwasiliana na
wizara hiyo juu ya mikataba hiyo.
Alidai
kuwa Desemba 2001, Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa alikwenda Rome, Italia kwenye Mkutano wa SADC
na alipokuwa huko, ubalozi ulifanya mpango atembelee jengo hilo
lililopendekezwa kununuliwa kwa ajili ya ofisi ya ubalozi.
“Wizara
ya Mambo ya Nje ya Italia ilifanya mipango yote kwa kumpa utaratibu na
usalama Kikwete ambapo alikwenda kutembelea jengo hilo na kukutana na
mama mwenye jengo,” alidai Profesa Mahalu.
Alidai
kuwa kabla ya mazungumzo na mwenye nyumba, mtoto wa mama huyo, Alberto
alimtembeza Kikwete kwenye jengo hilo ndani na nje na baadaye mazungumzo
hayo yaliendelea.
Balozi
Mahalu alisema baadaye mazungumzo kati ya Kikwete na mama huyo
yaliendelea na Alberto alikuwa akitafsiri, kwa sababu mama yake
hakufahamu lugha ya Kiingereza.
Profesa
Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimwuliza mama
huyo: “Hivi ni kwa nini kunakuwa na mikataba miwili?” na mama huyo
alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei
nafuu.
Profesa
Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo, Kikwete
hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha
kuhusu malipo ya awali ya dola milioni moja za Marekani ambapo aliafiki
na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka 2001.
Profesa
Mahalu alidai pia kwamba Kikwete alimweleza mama huyo kuwa
atalishughulikia suala hilo baada ya kurejea Dar es Salaam na kumshukuru
kwa kuwauzia jengo zuri.
Baada
ya kutoa maelezo hayo, Profesa Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete
kusema maneno hayo, alimgeukia na kumwambia: “Costa ni vizuri tupate
hela tumlipe huyu mama watu wengine wasije wakachukua hili jengo.”
Profesa
Mahalu alidai kuwa baada ya Kikwete kumshukuru mama huyo kwa ukarimu
wake, alimkaribisha Tanzania awe mgeni wa Wizara ya Mambo ya Nje yeye na
mumewe na kwamba watampeleka Ngorongoro.
“Tulipokuwa
njiani tukirudi hotelini alipofikia Kikwete akiwa kwenye gari alimpigia
simu Kibero akimuagiza afanye utaratibu wa kulipa Dola milioni moja
kama malipo ya awali ya jengo hilo,” alidai Profesa Mahalu.
Alidai
kuwa baadaye alimwagiza (Profesa Mahalu) aje Dar es Salaam kufuatilia
mpango huo wa malipo ya awali ya ununuzi wa jengo hilo.
Awali,
Profesa Mahalu akiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa alidai kuwa
anaitambua ripoti ya uthamini wa jengo hilo la ubalozi nchini Italia
uliofanywa na Kimweri kutoka Wizara ya Ujenzi aliyekwenda Rome Julai 15
hadi 26, 2001 kwamba jengo lilikuwa na gharama ya Sh6 bilioni.
Soma zaidi www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment