Thursday, February 9, 2012

MATOKEO KIDATO CHA NNE: JINSI MWANAFUNZI ALIVYOANDIKA BONGO FLEVA KWENYE MTIHANI



.
Baraza la mitihano la Taifa (NECTA) limewafutia matokeo yao watahiniwa elfu 3,303 baada ya kugundulika kufanya udanganyifu na kutumia lugha chafu kwenye mitihani yao ya kidato cha nne iliyofanyika oktoba 2011 ambapo katika hali isiyo ya kawaida mmoja wa watahiniwa hao aliamua kuandika katika karatasi yake wimbo wa bongo fleva.
Katibu mtendaji mkuu wa baraza hilo Dr Joyce Ndalichako amesema mmoja kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo alifikia hatua ya kuandika mashairi ya bongo fleva baada ya kukosa cha kujibu ambapo aliandika “nashukuru sana wote wanaosahihisha huu mtihani wangu, nitakapofeli nitaendelea na fani yangu ya bongo fleva, majita yangu yako levo za juu na sio East zuu, ukiona vyaelea ujue vimeundwa”
Joyce amesema mtahiniwa aliandika mistari katika kila sehemu alipotakiwa kujibu swali, swali la sita na la saba aliandika hiyo mistari hapo juu, swali la kumi na moja ameandika “acha utani my girl, unauja nyumbani umezizi, mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”
kwenye sentensi nyingine Katibu huyo mkuu amesema “katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana watahiniwa laki mbili na elfu 25 sawa na asilimia 53.37 wamefaulu huku kati yao wasichana ni elfu 90 na 885 sawa na asilimia 48.25 na wavulana ni laki moja na elfu 34 sawa na asilimia 57.51.
Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Francis Mbeya imeongoza kwa shule kumi zilizofanya vizuri, ambapo katika wanafunzi waliofaulu vizuri sana wameongozwa na Moses Andrew Swai kutoka shule ya sekondari ya Feza iliyopo jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment