Tuesday, February 14, 2012

MJUE ADOLF HITLER

Hitler


Muhtasari

 Adolf Hitler akiwa mtoto mchanga.




Tangu 1921 aliwahi kutokea kama kiongozi wa chama cha NSDAP (Nationalsozialistische Deutsche Arbeiterpartei - Chama cha Kizalendo - Kisoshialisti cha Wafanyakazi Wajerumani) inayojulikana pia kama Chama cha Nazi (tamka: natsi) chenye itikadi ya siasa kali na ubaguzi wa kimbari, swastika ikiwa ndiyo alama yao.
Alianzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu" akipiga marufuku vyama vya upinzani. Alitesa wapinzani wote na hasa watu wenye mbari aliyochukia Wayahudi.
Siasa yake ilianzisha 1939 Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wa Ulaya takriban milioni sita pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti.
Picha:AHWatercolor1.jpg
Picha iliyochorwa na Adolf Hitler inaonyesha mji wa Laon (Ufaransa).

Utoto

Alizaliwa Austria 1889, aliingia shule ya sekondari 1900 hakufaulu hivyo kushindwa kuendelea na masomo. Alijaribu tena kurejea shuleni zamu hii katika shule ya uchoraji iliyojulikana kama Vienna Academy of Fine Art huko Viena akafeli tena. Baada ya kifo cha wazazi alikosa usaidizi wa familia akakaa kwa muda katika nyumba kwa watu wasio na makazi.

Mwanajeshi 1914 - 1918

1913 alihamia Munich katika jimbo la Bavaria (Ujerumani). Katika Agosti 1914 wakati wa mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia alijitolea kwa jeshi la Bavaria alianza kwa kujitolea na kutokana na bidii na ukakamavu alipanda cheo na kuwa (praiveti). Mwisho wa vita mwaka 1918 alikuwa na cheo cha koplo.

Siasa

Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipaji chake cha kuhutubia watu. Akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi alikopanda ngazi haraka. Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini kiongozi wa kifashisti wa Italia aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano ya wafuasi wake kuelekea Roma.

Jaribio la mapinduzi 1923

Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria -kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin- lakini alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano lakini alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku.

Adolf Hitler (kulia) pamoja na dikteta wa Italia Benito Mussolini
Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf" ("mapambano yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia itikadi yake ya chuki dhidi ya Wayahudi. Hitler kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai ya kwamba kuna mbari (au: rangi) mbalimbali kati ya watu wenye tabia na thamani tofauti sana. Katika itikadi hiyo mbari wa juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria", wale ambao ni duni ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati juu au duni. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hii ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria.

Kujenga chama

Baada ya kutoka gerezani alirudi katika siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano na . Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia. Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS" ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi.
Chama chake hakikufaulu hadi 1929 wakati uchumi wa dunia pia Ujerumani uliporomoka vibaya. Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa. Katika hali hii watu walianza kupigia kura vyama vikali. Katika uchaguzi wa 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu. Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% na kuwa chama chenye kura nyingi. Katika hali hii viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933.

Chansella na kiongozi wa Ujerumani

Tarehe 30. Januari 1933 Hitler akawa Chansella wa Ujerumani. Alichukua nafasi mara moja kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani. Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa katika makambi ya KZ.
Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika ya kwamba uchumi wa dunia ukapoa tena. Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyopakana ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 pekee na akajenga jeshi kubwa.

Siasa dhidi ya Wayahudi

Chuki dhidi ya Wayahudi alionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi polepole. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milioni 62. Kila Mjerumani alitakiwa kuonyesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo. Kwa njia hii Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria" (hakuna Wayahudi katika familia), "Wayahudi" wa asili ya Kiyahudi, (hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi au hawakufuata dini), "Wayahudi nusu" kama mzazi mmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwa katika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali. Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili. Tokeo mmoja la siasa hii ilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwendo huu uliongezeka.

Vita Kuu ya Pili

Hitler alifuata siasa ya kukusanya Wajerumani wote katia Dola la Ujerumani. 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Uceki bila upingamizi wa kimataifa. Aliposhambulia Poland 1939 tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza na Ufaransa walisimama imara kwa mikataba ya usaidizi na Poland.
Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake.
Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote. Hitler alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa swali ya Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee. Baadaye siasa ya kuwatendea Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga kwa Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti.

Gazeti la Marekani "Stars and Stripes" la tar. 2.05.1945 latangaza kifo cha Hitler

Mwisho wa vita na kifo

Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler. Tarehe 20. Julai 1944 alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberg lakini hakuuawa.
Mwisho wa vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi ilikuwa imeshaingia mjini. Tarehe 30 April alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva Braun (alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi". Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi kutokana na meno yake.

            ****************MWISHO***************

No comments:

Post a Comment