Maajabu ya mwanaume mwenye
miguu mirefu duniani
Kijana Carl Griffiths, 19,
ndiye mwanaume mwenye mwenye miguu mirefu duniani. Kituko ni kwamba
anatumia ukubwa wa miguu yake kunasa wanawake.
Carl, raia wa Uingereza,
amesema kuwa mpaka sasa ameshatoka kimapenzi na wanawake 30 ambao
walidata kwake kutokana na urefu wa miguu yake.
Amesema kuwa wanawake wengi
wanavutiwa naye kwa kuamini kwamba ana kitu cha ziada kwenye mapenzi
kutokana na ukubwa wa miguu yake.
Pamoja na umri mdogo alionao,
miguu ya Carl ina ukubwa wa ‘saizi’ namba 21, ikiwa ni mara mbili zaidi
ya kipimo cha miguu ya wanaume wa kawaida nchini Uingereza.
Kwa kawaida, Waingereza miguu
yao ni namba tisa na wale wenye mikubwa, hufikia namba 10, kwa hiyo
umbile la miguu ya Carl ni ajabu kutokea.
Kutokana na hali hiyo, Carl
hutoa oda maalum kwa ajili ya kutengenezewa viatu vyake.
Carl, ambaye anaishi
Trimsaram, kusini ya Wales, Uingereza, amekuwa akichati kwenye mitandao
ya kijamii inayozungumzia wanaume wenye miguu mikubwa na kutoa siri zake
mbalimbali.
Akitoa siri zake, Carl
alisema: "Wanawake wamekuwa wakinitaka mimi kwa kitu kimoja tu, kwa hiyo
hawanisumbui.
Carl alisema, miguu yake ni
mikubwa mno na hakumbuki ilianza kukua lini.
“Ilikua kwa haraka mno,
nilipokuwa shule mama alikuwa anahangaika kuninunulia viatu vipya kila
mwezi . Kila mwaka nilikuwa nanunuliwa pea mbili au tatu.
"Nilipokuwa na umri wa miaka
12, nilikuwa navaa namba 14 ya viatu. Miaka miwili baadaye, nilikuwa
navaa namba 17. Nilikuwa nacheza mpira na nimehangaika sana kutafuta
buti la kuchezea soka mpaka nilipotengenezesha oda maalum kutoka
Marekani.”
“Kila kiatu huwa nalipia
pauni 100 (shilingi 270,000), pauni 50 ninapotoa oda na pauni 50 hulipa
ninapoanza kuvaa.
“Kwa sasa nina pea moja ya
mazoezi na nyingine kwa ajili ya kazi. Mara nyingi nikiingia klabu, watu
huacha mambo yao na kuniangalia mimi. Watu wanaopita jirani yangu,
hunikanyaga lakini huwa sijali.”
Baba wa Carl, Griffiths
mwenye umri wa miaka 39, alisema: “Sijui mwanangu amepata wapi hii miguu
kwa sababu hajanifuata mimi wala mama yake.”
No comments:
Post a Comment